KILIMO CHA MMEA WA MBONO
KUHIFADHI ARDHI NA KAMA
ZAO LA BIASHARA


Imetayarishwa December 2000 Na
Mradi wa Nishati mbadala kwa maendeleo ya akina mama
P.O Box 13954, Arusha - Tanzania.

KILIMO CHA MMEA WA MMBONO KUHIFADHI ARDHI NA KAMA ZAO LA BIASHARA

Utangulizi.
Mmea huu huitwa mbono pori au mchimba kaburi. Ni aina ya mti uotao na kustawi katika nchi za kitropiki. Una tabia za kustahimili ukame na huota katika maeneo yaliyoathirika kimazingira na yenye mmomonyoko wa udongo. Ukiota huweza kudumu zaidi ya miaka hamsini ukitoa maua na matunda ambayo hutoa mbegu zinazotoa mafuta.

MATUMIZI
Mmea huu una matumizi mengi. Miongoni ni kama kuzuia mmomonyoko wa ardhi, kuongeza bionuayi kwa kurutubisha udongo, kutoa mauwa ambayo huliwa na nyuki, kutoa mmbegu ambazo huzalisha mafuta yanayoweza kutumika kama nishati mbadala na sehemu za mmea huu ni dawa  ya matatizo mbalimbali.

KILIMO NA FAIDA ZAKE
Mti huu ukioteshwa vizuri unaweza ukawa uzio mzuri wa kudumu kuweka mipaka kwenye mashamba, viwanja na kukinga wanyama waharibifu wasiharibu na kushambulia mazao.

Hivyo basi Mbono ni mti wa kudumu kuzuiya mmomonyoko, Ni nishati mbadala, ni dawa ya asili na ni uzio wa kudumu kuzuiya wanyama waharibifu.

Jinsi ya Kulima.
Mahitaji na gharama zinazohitajika ili kuweza kulima, kupalilia kuvuna mmea huu sio kubwa na kukamua mafuta unaweza kutumia tekinolojia rahisi zilizopo vijijini kama vile ram press.

Hali ya hewa na udongo unaofaa.
Mmea huu unaweza kustawi kwenye maeneo yenye unyevu hadi maeoneo ambayo ni kame yenye mvua kati ya mm 480 hadi 2380.
Kwenye sehemu zenye mvua na unyevu wa kutosha mmea huu huendelea kutoa matunda wakati wote wa mwaka.

 


Utayarishaji wa mbegu na Vipandikizi
Unaweza kuotesha mmea huu kutoka kwenye mbagu au kwenye kipandikizi.

Mbegu: Tumia mbegu zilizokomaa na zilizojaa. Mbegu huota baada ya siku 9 na huanza kutoa matunda baada ya miaka mitatu had minne.

Kipandikizi: Tumia kipandikizi chenye urefu wa sm 45 - 100. Chimba mtaro wenye kina cha sm 30 na otesha vipandikizi hutoa mbegu baada ya mwaka mmoja.

Kupanda.
Nafasi
Otesha mita 2 kwa mita 2 ikiwa utanyeshea au mita 0.5 - 1.5 x 1-2 kwa kutegemea mvua kina sentimeta 2 - 3 na weka mbegu mbili kila shimo. Kupunguzia ni baada ya wiki 4.


Palizi.
Sio lazima kwani una asili ya kustahimili na kustawi porini bila palizi.

Uzalishaji.
Mmea mmoja huweza kutoa mbegu mfululizo kwa mwaka kwa sehemu zenye ukame huweza kuzaa mara mbili kwa msimu. Kiasi cha mbegu kilo 4 - 6 zinaweza kupatikana kwa kila mmea au tani 2 - 6 kwa mwaka kwa hekta.

Kuvuna.
Mbegu huvunwa kwa kuchunwa baada ya kukomaa kuiva na kukauka.

WADUDU NA MAGONJWA
Mmea huu haushambuliwi na magonjwa ila wasus wa aina ya vidudu vule hushambulia majani ambayo baadaye hupukutika.
 
KAKUTE - Kampuni ya Kusambaza Teknolojia inaendelez mirai ya kusaidia wakulima wadogo wadogo wa mazao ya mbegu za mafuta kama alizeti, ufuta, karanga kwa zaidi ya miaka sita nchini Tanzania.

Kampuni hii una wataalamu wenye uzoefu wa muda mrefu kwenye nyanja mbalimbali zikiwemo:

A) Teknoljia kwa miradi ya maendeleo vijijini.
      - Usindikaji wa mazao ya chakula.
      - Ujenzi wa nyumba za gharama nafuu.
      - Maji na mazingira safi.
B) Mafunzo na huduma za ushauri
C) Kuenesha na kusimamia miradi ya maendeleo
      Vijijini.

Mradi wa nishati mmbadala kwa maendeleo ya akina mama ulibuniwa mwaka 2000 ili kuendeleza na kusimamia zao la mmbono ili kuhifadhi ardhi na kuongeza kipato kwa akina mama.

Mradi huu unafadhiliwa na McKnight Foundation na kusimamiwa na HPI, KAKUTE Ltd walishirikiana na FAIDA na GEF Cross Boarder Project.

Kwa mawasiliano zaidi tuandikie au piga simu kwa anuanani hii:

KAKUTE Limited,
P.O. Box 13954;
Tel. 255 27 2544549
Email: kakute@tz2000.com
Arusha - Tanzania.

Back to Swahili Version

Back to Home